Hapa ndipo Baba wa Taifa alipozikwa. |
Nashukuru sana kupata nafasi hi ya kutowa heshima. Kwakweli najiona sasa ni mzalendo na Mtanzania Halisi |
Hapa ndipo walipozikwa wazazi wa Baba wataifa mwalimu JK Nyerere |
Mazingira mazuri nyumbani. Kweli ukiwa hapa unapata hisia kuwa mwalimu bado yuko |
Hili ndilo gari lamwisho Baba wa Taifa alilipanda -VX |
Hi sanamu mwalimu alipewa alipokwenda Ujerumani kama sijakosea |
Nikiwa na wadau |
Mwalimu alipenda mazingira sana |
Hi Nyumba ndiyo ile Baba Wa Taifa alijengewa na Jeshi letu. Aliishi ndani ya hi nyumba kwa siku 15 ndipo akaenda Uingereza kwa matibabu. |
Hapa ndipo mwenge wa uhuru unawashwa na kuzimwa. |
Nikishuhudia sehemu ambapo mwenge unapowekwa . Nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi tulikuwa tunakimbiza mwenge |
Nyumba ya mwalimu iko juu ya mlima |
Baada ya kustafu Mwalimu alikuwa anajishuhulisha na kilimo. na hapa ndipo alipokuwa anahifadhi mazao yake anayo vuna kama Mtama NK |
Sehemu yakuhifadhia mazao |
Nyumba ya Baba yake Mwalimu. Safi sana imetunzwa mpaka leo |
Mazingira tulivu na mazuri. |
Hi nyumba ndiyo ile mwalimu alijengewa na Chama cha TANU |
Mwalimu alihamia Digital toka 70s. Na hichi kingamuzi ndicho kilikuwa kina mpa habari toka sehemu mbalimbali duniani na yeye huwa alikuwa anasema kaoteshwa. Kumbe alikuwa anapata news hapa. Safi sana |
Nikaona namimi nitowe swagga labda nitaoteshwa |
Hapa ndipo mwalimu alipokuwa anapunga upepo. Basi ulikuwa ukisikia mtu kaitwa butiama kwa mwalimu ujuwe ndipo hapa alikuwa anabananishwa. |
Hapa ndipo mwalimu alipokuwa anaka kwenye kona |
Mwalimu alikuwa mtu wa dini |
0 comments: