Njiani kuelekea Kata ya Mvuha iliyopo katika Wilaya ya Morogoro (Vijijini)
Mwanasheria
Amani Mwaipaja akiwa katika picha ya pamoja na Aliyekua Mwenyekiti wa
Kijiji cha Mvuha (Morogoro Vijijini)Bwana Nyandikira muda mfupi baada ya
kuwasili Katika kata ya Mvuha
Jengo la Ofisi ya Kata ya Mvuha likionekana kwa mbali
Mto Mvuha (Uliopo Morogoro Vijijini) ukiwa umefurika katika kipindi hiki cha msimu wa mvua
Washiriki wakiwa katika majadiliano ya vikundi wakati wa semina
Habari Kamili
Mwanasheria
na Mtafiti Amani Mwaipaja ameanzisha program ya msaada wa kisheria kwa
jamii iishiyo pembezoni mwa nchi ya Tanzania (Vijijini) Kwa lengo la
Kuhamasisha Vijana-Wasomi kutumia Elimu na Rasilimali walizonazo katika
kufanya kazi za kujitolea kusaidia jamii. Program hiyo imepewa jina la
Jamii Kwanza.
Program ya
Jamii Kwanza inatoa semina, mafunzo na kusambaza elimu kwa njia ya
vitabu ili kuhakikisha kuwa jamii kubwa iishiyo vijijini inatambua haki
mbalimbali ilizo nazo kwa mujibu wa sheria za Tanzania
0 comments: